×

Meridianbet Yatoa Tabasamu Hospitali ya Kambangwa Kupitia Msaada wa Vifaa vya Usafi

Kampuni ya Meridianbet imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kugusa maisha ya watu na kuchangia ustawi wa jamii kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi katika Hospitali ya Kambangwa iliyopo Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika kupitia ushirikiano baina ya Meridianbet na uongozi wa Hospitali ya Kambangwa, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya hospitali na kuimarisha juhudi za kuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika mazingira safi na salama kwa wagonjwa, watumishi pamoja na wananchi wanaofika kupata huduma.

Katika tukio hilo, Meridianbet imekabidhi vifaa mbalimbali vya usafi ambavyo ni pamoja na buti (Boots), mifagio ya kusafishia sakafu (Big Mop), mapipa ya kutunza taka (Dustbins) pamoja na sabuni maalumu ya kuua vijidudu (Disinfectant Soap). Vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha shughuli za usafi na kuimarisha utunzaji wa maeneo yanayoizunguka hospitali hiyo.

Akizungumza kuhusu msaada huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesema kuwa kusaidia jamii zenye uhitaji ni miongoni mwa misingi muhimu inayoiongoza kampuni hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kushiriki katika kutatua changamoto zinazogusa maisha ya wananchi.

“Kuisaidia jamii na kugusa maisha ya watu wenye uhitaji ni sehemu muhimu ya misingi yetu. Tunaamini kuwa kampuni inaweza kuwa chombo cha kuleta mabadiliko chanya kwa kushiriki katika kutatua changamoto zinazozikabili jamii,” amesema Nancy Ingram.

Kupitia programu zake za CSR, Meridianbet imeendelea kutambua kuwa mchango wa kampuni kwa jamii hauishii katika shughuli za kibiashara pekee, bali pia unahusisha kushiriki katika juhudi za kuboresha maisha ya watu kupitia sekta mbalimbali, ikiwemo afya, mazingira na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Kwa habari na taarifa mbalimbali za michezo usisite kutembelea meridianbet ili upate mambo yote yanayotokea na kuendelea kwenye ulimwengu wakimichezo, ikiwemo michuano mikubwa ya Africa, Ulaya na ile ya falme za kiaarabu zote zinapatikana hapa.

Msaada huo kwa Hospitali ya Kambangwa ni sehemu ya jitihada hizo, ukilenga kuunga mkono kazi zinazofanywa na uongozi wa hospitali katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma. Meridianbet inaendelea kuonyesha kuwa mafanikio ya kampuni yana maana zaidi pale yanapoambatana na mchango wenye manufaa kwa jamii, kwa vitendo vinavyogusa maisha ya watu na kuleta mabadiliko chanya

Leave a Comment