
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi mpya za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato cha Nne, kwa ajili ya kujiunga na jeshi hilo katika kada mbalimbali.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Novemba 20, 2026, nafasi hizo zinahusisha waombaji wa Recruit Constable (Askari Mwanafunzi), pamoja na Janita Konstebo na Konstebo Mpiga Buruli.
1. SIFA ZA WAOMBAJI WA RECRUIT CONSTABLE (ASKARI MWANAFUNZI)
Waombaji wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na mwenye asili ya Tanzania.
b) Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na wenye asili ya Tanzania.
c) Awe amehitimu Kidato cha Nne mwaka 2024 au 2025, na Kidato cha Sita mwaka 2025 au 2026.
d) Kwa waombaji wa Kidato cha Nne, Kidato cha Sita pamoja na wenye Astashahada, wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
e) Kwa waombaji wa Kidato cha Nne wawe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Nne (Division I–IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa Daraja la Nne (Division IV), wawe na jumla ya alama 26 hadi 28.
f) Kwa waombaji wa Kidato cha Sita wawe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (Division I–III).
g) Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
h) Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi sita (5’6”) kwa wanaume, na futi tano na inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
i) Awe na kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
j) Awe na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.
k) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
l) Awe hajaolewa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
m) Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
n) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
o) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
p) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
q) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.
r) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
s) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
t) Kwa waombaji wenye elimu ya Shahada (NTA Level 8), Stashahada (NTA Level 6) na Astashahada (NVA Level 3), wanatakiwa kuwa na fani zilizoainishwa kwenye tangazo.
2. SIFA ZA JANITA KONSTEBO/KONSTEBO MPIGA BURULI
Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
i) Awe na umri wa miaka 18.
ii) Awe amehitimu Kidato cha Nne mwaka 2025.
iii) Awe na ufaulu wa Daraja la Nne (Division IV), wenye alama 26 hadi 28.
iv) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kupiga buruli na janita.
3. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Jeshi la Polisi limeelekeza kuwa waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao kupitia mfumo wa Ajira wa Polisi (Tanzania Police Force – Recruitment Portal), unaopatikana kupitia tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania: www.polisi.go.tz.
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe au kwa mkono hayatapokelewa.
Katika utaratibu huo, waombaji wanatakiwa kuwa na nyaraka na taarifa zifuatazo:
i) Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
ii) Namba za Index za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ambazo zitaingizwa kwenye mfumo wa ajira.
iii) Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na kuandikwa kwa anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, S.L.P 961, Dodoma, ikiwa na namba ya simu ya mwombaji. Barua hiyo inatakiwa kuwasilishwa kwenye mfumo katika mfumo wa PDF.
iv) Kwa waombaji wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada, wanatakiwa kuwasilisha jina la chuo walichosoma, namba ya usajili na mwaka wa kumaliza masomo.
v) Waombaji wanatakiwa kuwa na namba ya utambulisho wa Makazi (NaPA Number) kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata. Aidha, waombaji wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita watatakiwa kufanya usaili katika wilaya walikochukulia namba zao za NaPA.
4. MUDA WA MWISHO WA MAOMBI
Jeshi la Polisi limewataka waombaji wote kutunza majina wanayotumia kuingia kwenye mfumo (Username) pamoja na nywila (Password), kwa kuwa taarifa zote zinazohusu maombi yao ya kazi zitatumwa kupitia akaunti zao.
Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 30 Novemba 2026.
Tangazo hilo limetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, S.L.P 961, Dodoma, Novemba 20, 2026.
