
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya muundo wa Wizara mbili (2), uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali serikalini kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi wa Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amegawanya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa Wizara mbili ambazo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Aidha, amegawanya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa Wizara mbili ambazo ni Wizara ya Mifugo na Wizara ya Uvuvi.
Katika uteuzi na uhamisho wa viongozi, Rais Samia amefanya mabadiliko yafuatayo:
