×

Mahakama Yatangaza Nafasi za Kazi Mikoa Mitano, Mwisho wa Maombi Januari 15, 2027

Kwa mujibu wa Kanuni ya 4 na ya 6 ya Kanuni za Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama Na. 363 za Mwaka 2017, Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama pamoja na majukumu mengine, imepewa mamlaka ya kuteua madalali na wasambaza nyaraka wa mahakama. Kwa kanuni hizo, Mahakama ya Tanzania inapenda kuutangazia umma kuwa, kuna nafasi za kazi za Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama kwenye mikoa ya;

SIFA ZA MWOMBAJI

I. DALALI WA MAHAKAMA

i. Awe raia na mkazi wa Tanzania mwenye umri wa miaka kumi na nane na kuendelea;

ii. Awe mkurugenzi wa kampuni iliyosajiliwa Tanzania au mwendesha mnada mshirika katika taasisi ambayo imesajiliwa na kupewa leseni chini ya Sheria ya Waendesha Minada Sura ya 227 marejeo ya 2023;

iii. Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na uwezo kuzungumza lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha;

iv. Awe amehudhuria mafunzo ya majukumu ya madalali wa mahakama yanayotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) na kutunukiwa Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence);

v. Awe anafahamu kikamilifu kanuni za utekelezaji wa hukumu kama zilivyoainishwa na sheria ya mwenendo wa madai na sheria nyingine husika;

vi. Awe na tabia njema na muadilifu wa kiwango cha juu;

vii. Awe ni mtu mwenye ukwasi mzuri wa kifedha;

viii. Awe na kituo au ghala la kutosha kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa kwa ajili ya usalama; na

ix. Awe amelipa ada ya maombi ya kiwango cha shilingi 250,000/= ambayo haitarejeshwa.

KAZI ZA KUFANYA.

Kutekeleza tuzo na amri za mahakama zilizotolewa ndani ya mamlaka yake ambazo zinajumuisha: –

i. Kukamata na kuuza mali za mdai mhukumiwa (Judgment Debtor). Aidha, utekelezaji huo wa amri au tuzo zinazotolewa na mahakama lazima uzingatie sheria ya mwenendo wa madai na sheria nyingine husika;

ii. Kutekeleza amri za kuondosha mali, vitu au watu (eviction orders);

iii. Kutekeleza amri nyingine zozote zitolewazo na mahakama;

iv. Kuandaa na kuwasilisha taarifa namna utekelezaji ulivyofanyika kwa mahakama iliyotoa amri; na

v. Kutekeleza maelekezo mengine yoyote yatakayotolewa na mahakama.

II. MSAMBAZA NYARAKA WA MAHAKAMA

i. Awe raia na mkazi wa Tanzania mwenye umri wa miaka kumi na nane na kuendelea;

ii. Awe ana leseni kwa ajili ya kufanya kazi ya msambaza nyaraka wa mahakama.

iii. Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.

iv. Awe amehudhuria mafunzo ya majukumu ya msambaza nyaraka wa mahakama yanayotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) na kutunukiwa Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence).

v. Awe anafahamu kikamilifu kanuni za usambazaji nyaraka wa mahakama kama zilivyoainishwa na sheria ya mwenendo wa madai na sheria nyingine husika. na

vi. Awe amelipa ada ya maombi ya kiwango cha shilingi 30,000/= ambayo haitarejeshwa.

KAZI ZA KUFANYA

Kusambaza nyaraka za mahakama zinazotokana na mwenendo wa mashauri na zinazotolewa nje ya mwenendo wa mashauri ambazo zinajumuisha:-

i. Wito wa kuitwa shaurini, Taarifa, Nakala za Hukumu, Nakala za Maamuzi, Tuzo au Amri nyingine halali za Mahakama.

ii. Taarifa ya uteuzi wa Dalali wa Mahakama.

iii. Nyaraka nyingine zozote zitakazotolewa na Mahakama.

MAOMBI YA UDALALI

Mwombaji wa kazi ya udalali wa mahakama atapaswa kuandaa, na kupandisha (upload) kwenye mfumo nyaraka zifuatazo: –

i. Picha moja ya rangi (Passport size) iliyopigwa hivi karibuni;

ii. Nakala ya cheti cha kuzaliwa;

iii. Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV). (Taarifa isiwe na “Referees” ambaye ni ndugu jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji);

iv. Kivuli cha cheti cha elimu ya kidato cha nne na kuendelea;

v. Kivuli cha cheti cha umahiri (Certificate of Competence) cha majukumu ya dalali wa mahakama kilichotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) au chuo kingine kinachotambulika;

vi. Nakala ya Utambulisho wa mlipa Kodi (TIN);

vii. Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni ambayo mwombaji ataitumia;

viii. Leseni ya biashara kutoka katika Halmashauri ya Jiji, Mji, Manispaa au Wilaya;

ix. Nakala ya uthibitisho wa mlipa kodi (Tax Clearance Certificate);

x. Fomu ya wadhamini wawili wa mwombaji (Fomu Na. 5) yenye jumla ya kiwango cha udhamini kisichopungua milioni mia nne (Tshs. 400,000,000/=);

xi. Hati ya kubadilisha jina (Deed Poll) iwapo kuna tofauti ya majina katika nyaraka zitakazotumika katika maombi ya mwombaji;

xii. Taarifa ya Benki ya miezi kumi na miwili (12) ya hivi karibuni inayoonesha uwezo wa Kifedha wa kampuni itakayotumika au uwezo wa mwombaji;

xiii. Barua ya utambulisho ya Benki kuhusu akaunti ya mwombaji;

xiv. Leseni ya Udalali wa Kawaida (Auctioneers’ General License);

xv. Nakala ya hati hai ya bima ya moto, majanga na wizi;

xvi. MEMART (Memorandum and Articles of Association) ya Kampuni itakayotumika katika kazi ya Udalali; na

xvii. Uthibitisho wa umiliki wa ofisi, yadi na ghala la kuhifadhia bidhaa au mkataba wa upangishaji.

MAOMBI YA USAMBAZA NYARAKA

i. Picha moja ya rangi (Passport size) iliyopigwa hivi karibuni;

ii. Nakala ya cheti cha kuzaliwa;

iii. Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV). (Taarifa isiwe na mdhamini ambaye ni ndugu, jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji);

iv. Kivuli cha cheti cha elimu ya kidato cha nne na kuendelea;

v. Kivuli cha cheti cha umahiri (Certificate of Competence) cha majukumu ya dalali wa mahakama kilichotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA);

vi. Nakala ya utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN);

vii. Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni ambayo mwombaji ataitumia;

viii. Leseni ya biashara kutoka katika Halmashauri ya Jiji, Mji, Manispaa au Wilaya;

ix. Nakala ya uthibitisho wa mlipa kodi (Tax Clearance Certificate);

x. Fomu ya wadhamini wawili wa Mwombaji (Fomu Na. 5) yenye jumla ya kiwango cha udhamini kisichopungua Milioni mia nne (Tshs. 400,000,000/=); na

xi. Hati ya kubadilisha jina (Deed Poll) iwapo kuna tofauti ya majina katika nyaraka zitakazotumika katika maombi ya Mwombaji;

NJIA YA KUFANYA MAOMBI

Maombi ya kazi ya Udalali na Usambaza Nyaraka wa Mahakama yafanyike kupitia mfumo wa mahakama wa madalali (e-dalali) kupitia kiungo cha

https://edalali.judiciary.go.tz

MAELEZO MUHIMU

a. Mwombaji atakayepata changamoto katika kufanya maombi kwa njia ya mfumo, awasiliane na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi katika Mkoa aliopo kwa msaada zaidi.

b. Mwisho wa maombi ni tarehe 15 Januari, 2027 saa tano na dakika hamsini na tisa (5:59) usiku.

Imetolewa leo tarehe 24 Novemba, 2026 na: –

CHIGANGA M. TENGWAMSAJILIMAHAKAMA KUU YA TANZANIA

Leave a Comment