×

TFF Yatangaza Majina ya Awali ya Wagombea Uongozi Simba, Mangungu Akatwa


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza orodha ya majina ya awali ya wagombea waliofaulu hatua ya mchujo wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Simba SC.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, jumla ya wagombea wanne wameingia katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti, ambao ni Anindum Jonas Semu, Geoffrey Irick Nyange, Dkt. Seif Ramadhani Muba na Swedy Khamis Mkwabi.

Aidha, jumla ya wagombea 36 wameorodheshwa kuwania nafasi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, huku majina yao yakitajwa katika orodha iliyotolewa na kamati hiyo.

TFF imesema hatua ya kupokea mapingamizi dhidi ya majina ya wagombea hao itaanza Novemba 28 hadi 29, 2026, ambapo mapingamizi yatatumwa kupitia barua pepe ya [email protected].

Orodha hiyo ni ya awali na imetolewa baada ya mchujo wa fomu za wagombea wanaotaka kushiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Simba SC.

Leave a Comment