The House of Favourite Newspapers

Tiketi Al Masry Vs Simba Zazua Balaa, Watu Wavamia Polisi

 

TIKETI za mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Al Masry, zimezua kizazaa kikubwa.

Mashabiki wamekuwa wakipanga foleni kubwa kutaka tiketi na imeelezwa zimeisha.

Jambo hili linaonyesha kuwakasirisha mashabiki hao baada ya baadhi yao kwenda hadi katika baadhi ya vituo vya polisi na kulalamika.

 

Mashabiki hao wamelalamika kwamba wananyimwa tiketi pamoja na kufanya kila kilichotakiwa.

Jeshi la Polisi Misri katika mji huu ndiyo limekuwa likisimamia upatikanaji wa tiketi.

 

Watu walitakiwa kujiandikisha jina kamili, wanapoishi, picha zao, vyeti vya kuzaliwa na kadhalika na baada ya hapo unaingizwa kwenye mchakato wa tiketi kama utauziwa.

 

Lakini wengi wamekosa kwa kuwa haitakiwi idadi kubwa ya mashabiki kutokana na hofu ya vurugu baada ya Uwanja wa Port Said kuingia kwenye kashfa kubwa ya vurugu kutokana na zile vurugu zilizoua watu kwenye uwanja huo miaka michache iliyopita.

STORI: SALEH ALLY, PORT SAID | CHAMPIONI JUMAMOSI

Comments are closed.