The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga Ampa Makambo Mabao 30

Heritier Makambo.

WAKATI Jumatano ijayo Ligi Kuu Bara ikitarajiwa kuanza, tayari Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Heritier Makambo atafunga mabao 30 na kuwa mfungaji bora.

 

Mpaka sasa Makambo ameichezea Yanga mechi mbili za kirafiki wakiwa mkoani Morogoro na amefunga mabao mawili.

 

Kutokana na hali hiyo, Zahera amewataka mabeki wa ligi kuu watakaokuwa wakikutana na Makambo wajiandae kukabiliana na mziki wa mshambuliaji huyo ambaye kiwango chake kimekuwa kikiongezeka kila siku.

 

Zahera ameliambia Championi Jumamosi kuwa, licha ya Makam­bo kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kabla ya kujiunga na Yanga, sasa amekuwa akimpa mazoezi makali ambayo yanamfanya awe fiti, hali inayomfanya aseme mche­zaji wake huyo atafunga mabao 30 na kuwa mfungaji bora.

 

“Maendeleo ya Makambo siyo mabaya, anaendelea vizuri na kiwango chake kinaongezeka kila siku. Atakuwa na msaada mkubwa sana katika kikosi changu na tayari ameonyesha kuelewana vilivyo na Mrisho Ngassa, kwa hiyo mabeki wajipange kwelikweli.

 

“Kwa namna ninavyomfahamu na nimuonavyo hapa mazoezini ninaamini anaweza kufunga ma­bao 30 peke yake kama hatapata majeraha, kwa hiyo naamini pia anaweza kuwa mfun­gaji bora, subiri ligi ikianza mtaona makali yake,” al­isema Zahera.

 

Naye Makambo amesema kuwa yupo tayari kuipigania timu yake lakini ame­omba apewe mechi nne tu kwani kwa sasa mwili wake haupo fiti, baada ya hapo ataanza kuonyesha makali yake.

 

“Naendelea vizuri, nam­shukuru Mungu na sasa nipo fiti ila ili niweze kuwa sawa kabisa nahitaji mechi tatu au nne hivi kwani mwili sasa ni kama umech­acha kutokana na mazoezi magumu niliyokuwa nafanya kwa ajili ya kuwa fiti.

 

“Baada ya hapo naamini nitakuwa katika kiwango changu ambacho nakijua mwenyewe, tofauti na cha sasa.”

Comments are closed.