The House of Favourite Newspapers

Coastal Union kuikazia Simba leo

KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa wamejipanga kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.

Coastal Union wana kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani kwa kufungwa mabao 2-1 hali iliyowafanya wapoteze pointi tatu wakiwa nyumbani.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mgunda alisema; “Ninaitambua Simba ni timu kubwa na wana wachezaji wenye uzefu ila hilo hainipi taabu kwa kuwa ni timu inayofungika na mbinu zao tayari nimeshazijua.”

“Nimewapa kazi ngumu mabeki kuzuia kasi ya mashambulizi ya Simba na pia nimewapa kazi ngumu washambuliaji kuliandama lango la mpinzani lengo ni kupata pointi tatu, mashabiki sapoti ni muhimu,” alisema Mgunda.

Coastal Union imecheza jumla ya michezo 33 ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi zao 41 huku Simba ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 30 ina pointi 78.

Comments are closed.