The House of Favourite Newspapers

KIBABAGE WA MTIBWA SUGAR AMFUATA MSUVA DIFAA HASSANI EL JADIDA

Nickson Clement Kibabage akiwa na jezi ya timu yake mpya ya Difaa Hassani El Jadida

UONGOZI wa timu ya Mtibwa Sugar umesema kuwa mchezaji wao Nickson Clement Kibabage anataraji kujiunga na Difaa Hassani El Jadida msimu ujao 2019/2020.

Kibabage ameingia makubaliano ya miaka ya 4 kuitumikia Difaa El Jadida (2019-2023).

Difaa Hassan El Jadida na Mtibwa Sugar Sc tayari tumekubaliana juu ya uhamisho huu wa Kibabage ambaye alibakiza mwaka mmoja wa kuitumikia Mtibwa Sugar SC.

Kibabage atakuwa mchezaji wa pili kuitumikia El Jadida akiungana na Simon Msuva ambaye naye anatokea Tanzania.

Comments are closed.