The House of Favourite Newspapers

Wanaomchafua Muna Mungu Atadili Nao

UMESHAWAHI kuona mtu mwenye imani kiasi cha kuamini anaweza kuhamisha mlima? Basi mwigizaji Bongo Muvi, Rose Alphonce ‘Muna’ ametamba kuwa na imani hiyo kiasi cha mtu yeyote atakayemchafua, basi Mungu ndiye atadili naye.

Muna ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa wakimjadili wakimhusisha na mambo mabaya ili kumchafua, lakini alichoamua ni kutobishana nao na badala yake anamuachia Mungu.

 

“Watu wengi wamenichukulia kama jalala, lakini tangu nimeokoka nimemjua Mungu vizuri na yeye ndiye atadili na wote wanaonichafua kwa kuninenea,” alisema Muna.

Comments are closed.