Griezmann Apata Dawa ya Messi

ANTOINE Griezmann amedhihirisha atakuwa tiba ya tatizo la Barcelona kumtegemea kupitiliza staa wao, Lionel Messi. Mfaransa huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu, alipachika mabao mawili wakati timu hiyo ilipoicharaza Real Betis mabao 5-2 kwenye mechi ya La Liga, wikiendi iliopita.

 

Barcelona iliingia katika mchezo huo ikiwa na mapungufu kwenye fowadi yake kutokana na kuwakosa mastaa wake, Luis Suarez, Lionel Messi na Ousmane Dembele, ambao ni majeruhi.

 

Kumbuka Barcelona ilikuwa imepoteza mchezo wa kwanza baada ya kulizwa na Athletic Bilbao bao 1-0, ambapo pengo la Messi lilionekana wazi.

 

Messi ndiyo tegemeo la Barcelona likija suala la kupachika mabao na kutoa asisti katika timu hiyo. Kutokana na hali hiyo, Griezmann ndiyo alikuwa amebeba matumaini ya Barcelona na aliiongoza kutoa dozi hiyo kubwa dhidi ya Betis huku akishirikiana na mastaa wengine wa timu hiyo, Carles Perez, Rafinha Alcantara, Sergio Busquets na Jordi Alba.

 

Macho kwenye mchezo huo yalikuwa kwa Griezmann, ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Atletico Madrid. Griezmann alikuwa moto kwenye mchezo huo huku akionyesha makali katika ufungaji na pia kuwachezesha wenzake. Alifunga bao la kwanza na pili la timu yake.


Loading...

Toa comment