The House of Favourite Newspapers

Taifa Stars Yarejea Kishujaa Dar, Baada Ya Kutinga CHAN (Picha +Video)

TAIFA Stars imewasili leo Jumamosi, Oktoba 19, 2019 ikitokea nchini Sudan ambapo imerejea kishujaa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan ambao walitamba walipokuwa uwanja wa Taifa kwa kupata ushindi wa bao 1-0.

 

SELEMAN Matola, Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema kuwa kilicho nyuma ya ushindi wa timu ya Taifa ni kujituma na juhudi za wachezaji kutambua umuhimu wa mchezo wao dhidi ya Sudan uliochezwa jana nchini Sudan.

Matola amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kupata matokeo mbele ya Sudan kwani mchezo ulikuwa mgumu na kila timu ilikuwa inatafuta ushindi ili kusonga mbele kwenye hatua ya Fainali ya Michuano ya Chan 2020 nchini Cameroon.

“Kila timu ilikuwa na lengo moja kupata matokeo chanya  nasi pia tulikuwa tunafikiria jambo hilo, mchezo ulikuwa mgumu na ndiyo maana makosa yetu yalitufanya tuende mapumziko tukiwa nyuma, mwisho wa siku tulirekebisha makosa na tukapata ushindi.

 

“Mapokezi ya watanzania ni faraja kwetu na inaonyesha namna gani tumefanya kitu kikubwa kwa ajili ya Taifa hii ni rekodi kwetu na tuna kila sababu za kuwashukuru mashabiki pamoja na wadau kwa sapoti yao ya hali na mali tangu mwanzo na mpaka hapa tulipofika,”amesema.

Erasto Nyoni, beki mkongwe ndani ya Stars amesema kuwa ni furaha kwa mashabiki na taifa kiujumla kwa matokeo waliyopata kwenye mechi ngumu waliyocheza.

“Tunafurahi na shukrani zote ni kwa Mungu kwa kuwa yeye ndiye muweza wa yote, kwa sasa ni mwanzo wa kutazama hatua nyingine kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, kikubwa ni sapoti,” amesema.

 

Comments are closed.