×

Kilichompa tuzo Sven wa Simba Hiki Hapa

Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck akikabidhiwa tuzo ya Kocha Bora wa mwezi Februari 2020

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ametwaa tuzo yake ya kwanza ya kuwa Kocha Bora kwa mwezi Februari akiwashinda wenzake wawili ambao ni Hitimana Thiery wa Namungo FC na Abdul Mingange wa Ndanda FC kwa kufungwa mabao matatu huku wenzake wakifungwa mabao manne.

 

Simba, Februari imecheza mechi saba sawa na dakika 630 na imeshinda mechi sita na kupoteza mechi moja kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

 

Kwenye msako wa pointi 21, amepoteza pointi tatu na kukusanya pointi 18. Ameshuhudia mabao 12 yakifungwa na wachezaji wake huku mabao matatu yakiokotwa nyavuni kwa mlinda mlango wake.

 

Matokeo: Simba 2-0 Coastal Union, Simba 2-1 Polisi Tanzania, Simba 0-1 JKT Tanzania, Mtibwa 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba, Simba 1-0 Kagera Sugar, Simba 3-1 Biashara United.

 

Thiery wa Namungo, Februari alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi nane sawa na dakika 720, alishinda tano na sare tatu, akiwa anasaka pointi 24 aliambulia pointi 18 na kuyeyusha pointi sita. Timu yake ilifunga mabao 11 na kufungwa mabao manne.

 

Matokeo yake: Namungo 3-0 Mbao, Namungo 1-1 Alliance, Ndanda 0-0 Namungo, Singida United 0-1 Namungo, Mwadui 1-1 Namungo, Namungo 2-1 KMC, Namungo 1-0 Azam FC, Lipuli 1-2 Namungo. Mingange wa Ndanda FC mchezaji wake, Vitalis Mayanga ameibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari, alikiongoza kikosi chake kwenye mechi nane, alishinda tano, sare mbili na alipoteza moja mbele ya Mtibwa Sugar.

 

Kwenye pointi 24 alizokuwa akisaka ameambulia 17 na kuziyeyusha saba. Wachezaji wake walifunga mabao 10 huku wakifungwa mabao manne. Matokeo yake: Ndanda 1-0 Alliance, Ndanda 3-0 Mbao, Ndanda 0-0 Namungo, Mwadui 0-2 Ndanda, Singida United 0-1 Ndanda, Ndanda 1-1 Azam FC, Ndanda 2-1 KMC, Mtibwa Sugar 2-0 Ndanda. Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

 

Leave a Comment