The House of Favourite Newspapers

 50 CENT AMKATAA MWANAYE

RAPA kutoka Marekani, 50 Cent ameingia kwenye headline kwa mara nyingine baada ya kumkana hadharani kijana aitwaye Marquise Jackson (21) anayedaiwa kuwa ni mtoto wake.  50 Cent kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa kijana huyo siyo mtoto wake na tayari ameshapima damu kuhakikisha hilo.

“Yule sio mtoto wangu, Nimeshapima damu. Nitolee ujinga wako hapa,“ameeleza 50 Cent kwa kumjibu shabiki yake ambaye aliuliza kwa nini? 50 Cent kwenye shoo yake na Snoop Doggy walimbania dogo Marquis Jackson asiingie backstage na kumuacha nje kwenye viti vya kawaida.

Mwaka jana kijana Jackson, aliposti picha na akiwa na mtoto wa Supreme McGriff ambaye ni hasimu wa 50 Cent kwa muda mrefu, jambo hilo lilimkwaza mkali huyo wa Hip Hop na kushindwa kuzuia hisia na kukomenti kwenye posti hiyo kwa kuandika;” Hata kama watu hawa wawili wakigongwa na gari, kwangu haitakuwa siku mbaya.”

NEW YORK, MAREKANI

Comments are closed.