×

Polisi Dar Wakamata Wauza Shisha, Majambazi & Silaha (Video)

daladala1-1Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

daladala1-2Baadhi ya bastola zilizokamatwa.

daladala1-3
Sirro akiwaonyesha wanahabari bastola walizozikamata.

Na Denis Mtima, /Gpl

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumnasa mtu anayedhaniwa kuwa jambazi, anayefahamika kwa jina moja la Shomali, ambaye pia anatajwa kuhusika na mauaji yaliyofanyika kwenye daladala maeneo ya Tandika-Tambuka Reli jijini Dar hivi karibuni.

Shomari alikamatwa eneo la Tandika Maguruwe, akiwa na bastola aina ya Revolver ikiwa na risasi mbili ambapo katika purukushani za kumkamata, polisi walilazimika kumpiga risasi za mguuni wakati akijaribu kutoroka.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema katika tukio la kwanza, Kulwa Rajabu almaarufu Mamba, alikamatwa na askari wa kikosi maalum cha kuzuia ujambazi eneo la Mbande, Mbagala jijini hapa akiwa na silaha aina ya Browning ikiwa na risasi 12, baada ya kuwekewa mtego.
Baada ya kubanwa na polisi, Kulwa alitaja kwamba ameficha silaha nyingine, bastola aina ya Revolver ikiwa na risasi mbili, kwenye Msitu wa Dona, Yombo.

Kamanda Sirro aliendelea kueleza kuwa, pia jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata Ramadhani Abdi na Amiri Ally, eneo la Kariakoo baada ya kuvamia nyumbani kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Discount Centre, Sahim Mohamed na kupora fedha, laptop na vifaa vingine, kwa kutumia nguvu.