
Roma (kushoto) akisalimiana na mwanahabari wa Global publishers, Andrew Carlos (kulia) ndani ya Chumba cha Habari cha Global Publishers.




Roma akifanya mahojiano na wanahabari kwenye Chumba cha Habari cha Global Publishers.




Roma (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) pamoja na Msimamizi wa Masuala ya Burudani, Michale Izengo ‘Zagaro’.
Homa ya shoo ya nguvu ya “Nichane Nikuchane” inayotarajiwa kutimua vumbi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakheem kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya, Jumamosi hii Desemba 31, inazidi kupanda na katika kile kinachoonekana kama ni kujibu mapigo, mkali Ibrahim Musa ‘Roma’, ametamba kumfunika mkali wa ngoma ya Muziki, Shariff Thabeet ‘Darassa’.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye chumba cha habari cha Global Publishers, Bamaga-Mwenge leo, Roma amesema japokuwa watu wengi wanampa ushindi Darassa hata kabla ya mpambano wenyewe, atawaonesha kazi na anaamini kila mmoja ataelewa nani mkali kati yao.
“Hata mke wangu, mama Ivan anapenda sana nyimbo za Darassa, nikimjia juu ananiambia niache maneno niweke muziki, naamini hata yeye baada ya Shoo ya Chana Nikuchane, ataanza kunishabikia. Siwezi kusema nimejiandaa vipi lakini mashabiki wangu nawaambia waje kwa wingi Dar Live wataelewa kwa nini huwa najaza uwanja peke yangu,” alisema Roma.
Alipoulizwa atapanda na nani kusaidiana kupambana na Darassa, alisema hiyo ni siri yake na kuongeza kwamba ataimba nyimbo zake zote katika mtindo ambao mashabiki wake hawajauzoea kwa hiyo utakuwa ni usiku wa sapraizi kibao.
Na Hashim Aziz/ GPL