MTOTO wa Kocha wa Real Madr id, Zinedine Zidane, anayejulikana kwa jina la Enzo, juzi aliichezea timu hiyo mchezo wake wa kwanza na kufanikiwa kupachika bao muhimu kwa timu hiyo.
Real ilivaana na Cultural Leonesa kwenye mchezo wa Kombe la Copa del Rey, ambapo Enzo alifanikiwa kufunga bao hilo dakika 18 tu tangu aingie uwanjani.
Enzo ambaye kwa sasa na umri wa miaka 21, anaamini kuwa anaweza kuja kuwa mchezaji mahiri siku za usoni na alifunga bao hilo katika shuti lake la kwanza kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Madrid walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 6-1, ikiwa wamewachapa wapinzani hao wanaoshiriki Ligi Daraja la Pili kwa jumla ya mabao 13-2, baada ya kushinda 7-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Enzo ambaye ni mtoto mkubwa wa Zidane amefanikiwa kuichezea timu ya akiba ya Real michezo 50, huu ndiyo ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuichezea timu ya wakubwa.

