UHURU: Rais Magufuli amemaliza kuzungumza na Taifa, amesalimiana viongozi mbalimbali wa serikali na siasa na kuondoka kwenye Uwanja vya Uhuru jijini Dar, Sherehe za 55 za Uhuru wa zimefungwa rasmi.
JPM: Rais Magufuli amesema mwaka huu ndiyo wa mwisho kuadhimisha sherehe za uhuru jijini Dar, kuanzia mwakani sherehe hizo zitaadhimishwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
JPM: Amesema hakutakuwa na chakula wala Dhifa ya Taifa kama miaka mingine baada ya Sherehe za Maadhimisho ya 55 ya Uhuru yaliyofanyika leo Uwanja wa Uhuru, Dar.
JPM: Rais Magufuli amesema mwaka jana alikataza kuadhimisha sherehe za uhuru kwa kuwa ilikuw ni takribani mwezi mmoja tu tangu aapishwe, hakuwa ameteua Baraza la Mawaziri pamoja na watendaji wengine, licha hivyo gaharama za kufanikisha sherehe hizo zilikuwa kubwa kiasi cha Tsh Bilioni 4 wakati serikali haikuwa na pesa.
“Mambo mengi yalitakiwa kufanyika ikiwemo kulipa posho pamoja na chakula cha wageni, Je, chakula hicho wanakula wananchi wote? Jibu ni hapana, ndiyo maana nikaona nizifute. Amesema Rais Magufuli.”
JPM: Mpaka sasa tumenunua ndege 6.
JPM: Mafanikio ya Tanzania tangu kupata uhuru Desemba 9, 1961, Tumelinda mipaka yetu, wapo waliojaribu kutishia uhuru wetu lakini wameshindwa, hatubaguani kwa misingi ya rangi, kabila, vyama, tumeboreha miundombinu ya reli, barabara, afya na elimu namengine.
Changamoto.
JPM: Licha Umaskini, ukosefu wa huduma za jamii, ajira nakadharika. Tutajitahidi kutatua hizo changamoto ambazo tayari tumeanza kushughulikia.
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Vikundi vya Ngoma vinaendelea kutoa burudani uwanjani hapo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Askari mwanakikundi wa Kwata ya kimya kimya anatakiwa aishi kwa uzito usizozidi Kg 50. Akinenepa anatolewa kikundini.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: kikundi cha kwata ya kimya kimya kimemaliza maonesho na kinatoka nje ya uwanja.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Kikosi cha JWTZ kinafanya kwata ya kimya kimya.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Makomando wawili pekee wamesukuma gari la jeshi kinyume nyume kisha kulivuta tena kwa mikono yao.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Makomando wa Karate wa JWTZ wanaingia kuoneshamaonesho 9 ikiwemo ukakamavu wa mwili.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Makomando wamebeba mabegi yenye zana za kazi zenye kg 65, zinazowazwezesha kuishi kwa siku 7 bila kutegemea chochote
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Makomando wa Wanamaji na wa JWT wanaingia uwanjani kuonesha mbembwe zao.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Bendi imeingia uwanjani kutoa salamu zake kwa rais @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Gwaride limefikia tamati uwanjani na linatoka nje ya uwanja wa Uhuru, Dar zinapofanyikia sherehe hizo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Wimbo wa Taifa Unaimbwa
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Wakati Bras Band ya jeshi ikipigwa, Vikundi vya Gwaride vinapita mbele ya Rais @MagufuliJP na kutoa heshima zao.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Rais @MagufuliJP akisalimiana na viongozi wengine jukwaani.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Gwaride Rasmi la kuadhimisha Miaka 55 ya Uhuru linakaguliwa na Rais @MagufuliJP kwenye Uwanja wa Uhuru.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Kauli Mbiu ya Mwaka 2016 “Tuunge Jitihada Za Kupiga Vita Rushwa Na Ufisadi Na Tuimalishe Uchumi Wa Viwanda”.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Mizinga 21 inapigwa hivi sasa kama ishara ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt John pombe Magufuli anawasili uwanajani hapo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anawasili uwanjani hivi sasa.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Ali Mohammed Shein anawasili uwanjani hapo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ:Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa anasalimiana na viongozi mbalimbali waliofika
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa anawasili uwanjani hapo
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Athuman Chande anawasili uwanjani.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Rais Mstaafu wa awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongozana na mkewe.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Marehemu Abeid Karume, Mama Fatuma Karume anaingia uwanjani hapo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Karume amefika uwanjani akiongozana na mkewe mama Karume.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Tayari Kikundi cha Bendera Kimeingia Uwanjani.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#MIAKA_55_YA_UHURU_TZ: Gwaride limetoa heshima kwa viongozi waliofika kuhudhuria sherehe hizo.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016
#UHURU_TZ_55: Sherehe za Kuadhimisha Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania zimeanza rasmi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, gwaride lipo uwanjani.
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 9, 2016