Muuza sura kwenye video za Kibongo na msanii mpya wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva,’ akiwa Global TV Online leo kutambulisha wimbo wake wa kwanza wa Milele amemshirikisha Barnaba.
Lulu Diva akisoma meseji za mashabiki wake.
Akijiweka sawa kabla ya kufanya mahojiano na Global TV Online.
Mtangazaji wa Global TV, Kelvin Shayo (kushoto) akifanya mahojiano na Lulu Diva.
Kelvin Shayo akiendelea na mahojiano.
Akicheka baada ya kuulizwa kutaja wasanii wa kike na wa kiume anaowakubali.
Lulu Diva akimkabidhi CD ya wimbo wake wa Milele, Kelvin Shayo (kushoto).

Akiwa katika pozi baada ya mahojiano.
MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva, amegeukia upande wa pili wa Bongo Fleva kwa kuibuka na ngoma yake ya kwanza aliyomshirikisha Barnabas Elias maarufu Barnaba.
Wimbo wake huo umetungwa na msanii wa Bongo Fleva, Barnaba na kutengeneza katika studio ya Barnaba. Katika mahojiano na Global TV Lulu Diva amesema mashabiki wake waliomzoea kumuona katika video mbalimbali kwa sasa watarajie ngoma kali kutoka kwake kwa sasa ameanza na Milele na hivi karibuni ataachia video ya wimbo wake aliyoitengenezea Afrika Kusini. Ametumia zaidi ya milioni 40 kutengeneza ngoma hiyo.
Pia amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva ndani na nje ya nchi kudownload wimbo wake kupitia Mkito au Youtube.
