Darassa akisaini mkataba wa mpambano wa Nichane Nikuchane utakaofanyika Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live. Kulia ni Meneja wa Dar Live, Juma Mb i z o.
Darassa baada ya kusaini mpambano huo.
Mkali wa ngoma ya Muziki, Darassa akiwa katika pozi.
Darassa akipozi na Juma Mbizo.
Mwana Hip hop R.O.M.A akipitia mkataba wa mpambano wa Nichane Nikuchane kabla ya kuusaini.
R.O.M.A akimwaga wino tayari kwa mpambano huo wa Mwaka Mpya ndani ya Dar Live.

Mbizo naye akimwaga wino kwa niaba ya Dar Live.

Mbizo na R.O.M.A mara baada ya kusaini mkataba wa pambano. Kulia ni MC wa Dar Live, Dalada.
WAKALI wawili ambao hawashikiki kunako muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ na Shariff Thabeet ‘Darassa’, wamesaini mpambano wa Nichane Nikuchane utakaofanyika kwa mara ya kwanza Mkesha wa Mwaka Mpya (Desemba 31, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live u l i o p o Mbagala-Zakhem jijini Dar.
ILIKUWAJE?
Kwa kipindi kirefu mashabiki wa burudani walikuwa na hamu ya kuwaona wakali hao wakipanda jukwaa moja na kufanya ‘rap battle’ ambapo uongozi mzima wa Dar Live ukaona ni vyema u k a w a t a f u t a wakali hao na kuwasainisha kuingia katika mpambano huo unaokwenda kwa jina la Nichane Nikuchane.
R.O.M.A, DARASSA WATINGA GLOBAL
D a r Live ilifanikiwa kuwapata wakali hao ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita walitinga ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na kusaini kufanya mpambano huo unaotarajiwa kuwa wa kihistoria.
Akizungumza na tovuti hii, Meneja wa Dar Live, Juma Mb i z o, ali s e m a baada ya k u s a i n i mpambano huo, kilichobaki ni mashabiki kujitokeza kwa wingi Mkesha wa Mwaka Mpya kuburudika na shoo hiyo ambayo haijawahi kufanywa na wakali hao.
“Ni jambo la kumfurahisha kila shabiki wa muziki huu, lengo ni kuwaonyesha mashabiki muziki wa Hip Hop kwa sasa umerudi upya na kujenga heshima. Wale mashabiki wa R.O.M.A anayebamba na Ngoma ya Kaa Tayari na Viva Roma Viva wataburudika naye na hata mashabiki wa Darassa anayetamba na Too Much pamoja na Muziki nao watakata kiu yao.
“Utakuwa ni usiku wa Nichane Nikuchane, weka ngoma hii mi naweka hii ni kama kamchezo ka kuibiana mashabiki na wakati huohuo kuwapa burudani,” alisema Mbizo.
MSIKIE R.O.M.A
Akiizungumzia shoo hiyo, mkali R.O.M.A aliwataka mashabiki wa Hip Hop na muziki wa Bongo Fleva kujitokeza kwa wingi kushuhudia shoo atakayoifanya. “Hii si mara yangu ya kwanza kutimba Dar Live, safari hii nimesaini mpambano wa Nichane Nikuchane na kama mjuavyo sitabiriki na wala sijawahi kumuangusha shabiki yangu yeyote.
Mashabiki watapata kunisikia R.O.M.A wa kipindi hiki cha Magu (Magufuli) nikiwa katika ubora wa kipekee tofauti na vipindi vyote.
“Sipendi kuwa muongeaji sana, ila shoo zangu huwa zinaongea zenyewe. Usikose mwaka mpya kwenye michano nikiwa na debe lililojaa ngoma kama Ivan, Kaa Tayari, 2030, Viva
Roma Viva, KKK na nyingine kibwena,” alisema R.O.M.A.
DARASSA
Naye mkali wa Hip Hop anayetikisa kila kona na Ngoma ya Muziki, Darassa alifungukia siku hiyo kuwa, atawadhihirishia mashabiki wa Hip Hop na Bongo Fleva kwa ujumla kuwa Hip Hop itaendelea kudumu milele.
“Unapozungumzia Muziki wa Hip Hop kwa sasa, unazungumzia ngoma ya Muziki.
Nashukuru ngoma imeeleweka na imepokelewa kila kona ya nchi. Kikubwa nimeshasaini mpambano, hivyo tukutane pale Dar Live nikiikamua kwa mara ya kwanza katika kiwanja hicho.
“Najua mashabiki wamenimiss sana jukwaani hasa Dar Live, hivyo wanangu wote msikose kwani mbali na kuchana ngoma zangu kama Too Much, Heya Haye, Kama Utanipenda na nyingine nyingi, pia nimewaandalia sapraiz kibao,” alisema Darassa.
WENGINEO SASA!
Akizungumzia wakali wengine watakaokuwepo siku hiyo, Juma Mbizo alisema, mashabiki pia watarajie kuwasikia Makhirikhiri kutoka Tanzania na ID Classic.
“Pia tutakuwa na mkali wa Singeli, Msaga Sumu na kundi lisilo na mpinzani Bongo kunako muziki wa Taarab, Jahazi Modern chini ya Leyla Rashid na Amigo,” alisema Mbizo.
KRISMASI PIA SHOO YA KIBABE…
Mbizo alisema mbali na shoo hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya, katika kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, mashabiki wa burudani wameandaliwa shoo kutoka kwa mkali wa Soukous
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Matumona Francois maarufu kama General Defao.
Mkali wa Soukous kutoka DRC, Matumona Francois maarufu kama General Defao.
“Kuonyesha kuwa tupo karibu na wapenda burudani za aina zote, Dar Live itameremeta siku ya Krismasi kwa kuwadondoshea mkongwe wa muziki kutoka Kongo. Niwaambie tu,
Defao hajawahi kupafomu Dar Live na hii itakuwa mara yake ya kwanza na kizuri zaidi ataporomosha albamu yake mpya ya Time is Money iliyo na vibao vikali kama Mwami Rajabu,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa viingilio katika shoo zote vitatangazwa, hivyo endelea kufuatilia tovuti hii na Magazeti ya Global Publishers.







