MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli ameanika mambo 10 ‘pasua kichwa’ (yanayosumbua utendaji na utekelezaji wa mipango mbalimbali) ndani ya chama hicho na kuahidi kuyavalia njuga ili kukiimarisha chama.
Mambo hayo ameyaanika wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu Taifa ya CCM (NEC) leo, Desemba 13, 2016, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
10. Tunataka chama kinachowatumikia wanachama wote, na si cha wachache wa ngazi za juu, chama kiwafikie hadi wa chini- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
9. Tunataka chama kinachoongoza wanachama na si mwanachama anayeongoza chama. Mwanachama ndiye afuate chama- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
8. Vyeo ambavyo havijatamkwa na Katiba ya chama visiwepo, mfano mwenyekiti wa wenyeviti, Jumuiya ya Wazazi- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
7. Tunataka kiongozi mmoja ndani ya chama awe na nafasi moja ya uongozi ili kuwapa nafasi na wengine kukitumia chama- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
6. Tunataka kujenga chama kilichoimara kuanzia chini kwenye ngazi ya shina, matawi, kata, wilaya hadi ngazi ya taifa- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
5. Tunataka kuondoa wasaliti na makundi ndani ya chama. Kuna watu wanaendeleza makundi hata baada ya uchaguzi- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
4. Tunataka chama kijitegemee kiuchumi, tunavyo vitegauchumi vingi lakini tumekuwa ombaomba hasa wakati wa uchaguzi- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
3. Kuongeza wanachama haswa vijana kwani chama ni wanachama. Tunataka wanachama watakao kipenda chama na kulipa ada- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
2. Kujenga chama chenye nguvu cha kuwatumikia wananchi, sisi ndio tuliopewa dhamana hatupaswi kuwa walalamikaji- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
Malengo katika uongozi wangu kama Mwenyekiti wa CCM
1. Kuondoa mianya ya rushwa ndani ya chama, chama kimechafuliwa na rushwa- @MagufuliJP— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Sio kwamba sipati mialiko kwenda nje, nimepata mialiko karibia 50, lakini nilitaka kusafisha kwangu kwanza- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Tumeanza kurekebisha viwanja vya ndege, kujenga reli, barabara na madaraja ili tutimize tuliyoyaahidi- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Tutanunua meli mpya mbili ambapo moja itakuwa Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Victoria- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Hadi sasa serikali imenunua ndege sita mpya. Huwezi ukajenga uchumi wa utalii ukitegemea ndege za jirani- M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Wajumbe halali tu ndio wataruhusiwa kushiriki uchaguzi. Tukigundua kuwa kuna mapandikizi tutafuta uchaguzi – M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Hatutamsamehe mtu yeyote atakayetaka kuupata uongozi kwa njia ya rushwa kwani wametuumiza sana. – M/kiti Dk @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
#NECCCM Utaratibu wa uongozi wa CCM utaanza mwezi Februari 2017 na kukamilika mwezi Novemba 2017- M/kiti Dk @MagufuliJP

Kama vyama vingine navyo vinataka kuja kufanyia vikao Ikulu, waombe, lakini utaratibu ni kwamba lazima tujue watajadili nini.- M/kiti CCM pic.twitter.com/cMjvTbEmzb
— Global Publishers (@GlobalHabari) December 13, 2016
INASIKITISHA MAITI SITA ZAFUNGWA KWENYE VIROBA ZATUPWA MTO RUVU