×

CCM Yawateua Polepole Kuwa Katibu wa Itikadi & Uenezi, Mpogolo Naibu Katibu Mkuu Bara

polepole
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezikuchukua  nafasi ya  Nape Nnauye.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia ukurasa wake wa Twitter zinaeleza kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kimemteua Polepole kushika wadhifa huo.
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye anataraji kumkabidhi ofisi Hamphrey Polepole Disemba 15, 2016.
mpogoloRodrick Mpogolo
Halmashauri Kuu ya CCM imemteua aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato na baadaye mshauri wa Rais masuala ya siasa, Bwana Rodrick Mpogolo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Tanzania Bara, akichukua nafasi ya Rajab Luhwavi aliyeteuliwa kuwa Balozi
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kimefanyika leo ambapo miongoni mwa mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

magufuliii

Maamuzi ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM;

1. Kupunguzwa kwa idadi ya wajumbe na vikao vya chama vinavyofanyika kwa mwaka.

2. Wajumbe wa NEC wamepinguzwa toka 388 wa sasa hadi 159 ili kurahisisha ufanyaji wa maamuzi na wanachama kutotumia muda mwingi kwenye vikao

3. Vikao vya NEC vitafanyika mara mbili kwa mwaka (kila baada ya miezi 6) badala ya mara tatu (kila baada ya miezi 4)

4. Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wamepunguzwa kutoka 34 wa sasa hadi 24 huku vikao vikiwa baada ya miezi minne badala ya miwili ya awali.

5. Wajumbe watatu wa Kamati ya Siasa ya Mkoa watapungua na vikao ni kila baada ya miezi mitatu badala ya mwezi mmoja kama ilivyo sasa.

6. Wajumbe wanne wa Kamati ya Siasa ya Wilaya watapungua na vikao ni kila baada ya miezi mitatu badala ya mwezi mmoja kama ilivyo sasa.

7. Kuanzisha Shina la chama kutahitaji wananchama katika ya 50-300 tofauti na wanachama 5 wa awali, na kuanzisha Tawi ni wanachama 300-1000.

8. Vyeo ambavyo vimefutwa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya CCM. – M/kiti wa Wenyeviti wa Mikoa – Makamanda wa Vijana – Walezi – Washauri

9. Chama cha Mapinduzi kimepanga kufanya uhakiki wa wanachama wake ili kupata idadi kamili na pia kuanza kutumia kadi za kielektroniki.

10. CCM imeunda kamati maalum itakayokwenda Zanzibar kuchunguza hali ya kisiasa ndani ya chama na mchakato mzima wa uchaguzi.

11. Kuhusu wasaliti, ripoti kuhusu tathmini ya uchaguzi bado inafanyiwa kazi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote waliokisaliti chama.

12. Mabadiliko haya yaliyotajwa yatatekelezwa baada ya katiba na kanuni za chama kufanyiwa marekebisho na uchaguzi wa chama kufanyika.

halotel-strip-1-1

Alichokizungumza Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli kwenye kikao cha halmshauri kuu