×

Wajasiriamali Wafurika Semina Ya Wezesha Mzawa

semina-mbagala1-12  Meza kuu kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Kilimo na Ufugaji wa Samaki, mzee Moshi Macmillan, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani Professional, Hassan Ngoma na Mkurugenzi wa Mjasiriamali Kwanza, Dk. Didas Lunyungu.

semina-mbagala1-22Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo akitoa mada.

semina-mbagala1-21Eric Shigongo akiendelea na mada.

semina-mbagala1-23Wajasiliamari  kutoka viunga vya Jiji la Dar es Salaam wakimpokea  Eric Shigongo

semina-mbagala1-20Dk. Didas akizungumza na wajasiriamali.

semina-mbagala1-1 semina-mbagala1-2

semina-mbagala1-4Wajasiriamali  walijitokeza kwa wingi katika Semina ya Ukombozi wa Kiuchumi wakiendelea kusikiliza.

semina-mbagala1-3semina-mbagala1-5Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani Professional, Hassan Ngoma akitoa mada.

semina-mbagala1-6 semina-mbagala1-7 semina-mbagala1-8Mtaalamu wa Kilimo na Ufugaji wa Samaki, mzee Moshi Macmillan, akitoa somo kwa wajasiliamali (hawapo pichani).

semina-mbagala1-11Mhasibu wa Wezesha Mzawa Microfinance, Shamimu Mshana, akiwa kwenye meza ya vitabu vya Shigongo.

semina-mbagala1-14Maofisa wa Wezesha Mzawa wakifuatilia semina hiyo.

semina-mbagala1-16Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Deborah Masinde, akitoa burudani.

semina-mbagala1-17 semina-mbagala1-18 semina-mbagala1-19Baadhi ya wajasiriamali wakitoa ushuhuda.

semina-mbagala1-24Waimbaji MC Makondeko na Tumaini Njole wakitumbuiza.

Gabriel Ng’osha na Kasmir Mseleche/GPL

WAJASIRIAMALI kutoka viunga vya Jiji la Dar es Salaam, jana walijitokeza kwa wingi katika Semina ya Ukombozi wa Kiuchumi iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live ulioko Mbagala Zakhem jijini Dar.
Watoa mada katika semina hiyo walikuwa ni Mwezeshaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Mkurugenzi wa Mjasiriamali Kwanza, Dk. Didas Lunyungu, Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani Professional, Hassan Ngoma na mtaalamu wa kilimo, mzee Moshi Macmillan.
Watoa mada hao walitoa mada mbalimbali za namna ya kuinua uchumi katika utawala wa serikali ya awamu ya tano, namna ya kuanzisha viwanda vidogovidogo kama kiwanda cha sabuni, dawa ya kusafishia majumbani, kilimo mtambuka cha matikiti-maji, vitunguu, mbaazi, dengu, ufugaji wa samaki na ubunifu wa kutengeneza pesa katika biashara.
Mbali na mafunzo ya ujasiriamali, semina hiyo iliambatana na burudani kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za Injili, Deborah Masinde, MC Makondeko na Tumaini Njole.

MAKONDA ALIPOKUTANA NA MTOTO MWENYE ULEMAVU


halotel-strip-1-1