Na Denis Mtima
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi limesema kuwa liliamua kuruhusu kuzikwa kwa miili ya watu saba iliyokutwa pembezoni mwa Mto Ruvu, eneo la Makurunge wilayani Bagamoyo kati ya Desemba 6 hadi 9, 2016 kwa sababu miili hiyo ilikuwa imeharibika vibaya na ilikuwa ikitoa harufu, huku mmoja uliopelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ukishindwa kutambuliwa na ndugu zake.
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz, alisema wameamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuendelea kusambaa kwa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuhusu maiti hizo na uamuzi wa kuzizika haraka.
Wanahabari wakifuatiliatukio hilo.
“Kutokanana ukweli kwamba baadhi ya maiti hizo zilikuwa zimeharibika vibaya, iliamuliwa kwamba maitisita zizikwe katika eneo la tukio na moja yenye unafuu ilipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwenye chumba cha maiti hadi Desemba 16 ulipozikwa na halmashauri baada ya kutotambuliwa na ndugu yeyote,” alisema Kamanda Boazi.
Pia Jeshi la Polisi limesema linaendelea kumtafuta Benard Focus Saanane ambaye anadaiwa kupotea na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea na mwananchi yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwake, waziwasilishe kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu nao.
Pia amewataka wananchi kuwa watulivu kuhusu suala hilo wakati wakiendelea na upelelezi wa kina.
SHILOLE “MAMA YANGU ALIKUWA MAMA NTILIE NA ALITUSOMESHA”