×

Haji Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro, TFF

manara-na-muroAfisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara ameandika barua ya wazi kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamali Malinzi akimuombea msahama Afisa Habari wa Yanga, Jerry Muro aliyefungiwa kujihusisha na mpira wa miguu kwa mwaka mmoja.

Jerry Muro alipewa adhabu hiyo na TFF kufuatia matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari kosa alilolitenda mwezi Julai mwaka huu.

Manara kupitia ujumbe huo aliouweka kwenye ukurasa wake wa Instagram amemuomba Rais Malinzi kumfungilia Jerry Muro kwa alisema hata rudia na kwa vile ametumikia nusu ya adhabu yake basi anaamini amejifunza kutokana na makosa.

Isome hapa chini Barua hiyo ya Haji Manara kwenda wa Rais wa TFF.

*********************

Kwako Rais wa TFF

Kwanza nikutakie heri na baraka katika sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Ninakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi kwako nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini, kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo katika sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi nitakalokuomba.

Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambae TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake.

Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa ameshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla.

Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba.

Tuna-‘miss’ pilika zake zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. Kwangu Mh Rais nina hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.

Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Wako,
HAJI MANARA

ILIKUPITA HII?

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Cheki Video Akipika Msosi Gheto