×

Wadaiwa Sugu Elimu ya Juu Kuanza Kusakwa Nyumba Hadi Nyumba

vlcsnap-2016-12-28-12h44m13s191
Mkurugenzi Badru (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, leo

vlcsnap-2016-12-28-12h44m48s866

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu tanzania (HESLB), imesema itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha linawatafuta wadaiwa sugu ambao watashindwa kurejesha mikopo yao, baada ya tarehe ya mwisho, Desemba 31, 2016 kupita.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Abdulrazak Badru, alisema kiwango wa wadaiwa sugu waliojitokeza tangu walipotoa tangazo kwa mara ya kwanza, kinaridhisha ingawa bado wapo wengine wengi ambao hawajajitokeza hadi sasa.

Akaongeza kuwa, wote ambao hawajajisalimisha, bodi imeunda kikosi kazi ambacho kitawasaka popote walipo, hata ikibidi kupita nyumba hadi nyumba, kwenye baa, kwenye sherehe, kwenye nyumba za ibada na kila mahali walipo, ili warejeshe fedha walizokopeshwa kwa lengo la kuwanufaisha wanavyuo wengine.

Aidha, Badru alisema kuwa wanatoa siku kumi na nne kwa waajiri sugu, ambao hawakati kiwango cha asilimia 15 ya mishahara ya wanufaika wa mikopo, au kutowasilisha kiwango hicho kwenye bodi, kuhakikisha wanafanya hivyo ambapo watakaokiuka, watakuwa wanatenda kosa kisheria ambalo linaweza kusababisha wakakamatwa, wakapigwa faini au kufungwa jela.

Pia, Badru alisema wameongeza muda wa kuanza kulipa madeni kwa wanufaika (grace period) kutoka mwaka mmoja wa sasa mpaka kufikia miaka miwili. Amewataka wanufaika ambao hawapo kwenye ajira rasmi, nao kuhakikisha wanarejesha kiwango kisichopungua shilingi laki moja (100,000) kwa mwezi.

Na Kelvin Shayo/GPL