×

Pumzika kwa Amani Padri Lupondya na Watoto wa Utoto wa Yesu

padri-luopndya-1

padri-luopndya-2

padri-luopndya-3

padri-luopndya-4

padri-luopndya-5

padri-luopndya-6SHINYANGA: Maaskofu wa majimbo manne , mapadri , watawa na mamia ya waamini  wameshiriki misa ya mazishi ya Padri Andrew  Lupondya (33)  na watoto watano wa  Shirika Rafiki wa Utoto wa Yesu (VIFRA)  na mlezi wao Mama Judith  Kajwahula (63 )  wa Jimbo Katoliki Kahama waliofariki  katika ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokana na gari walilokuwemo kugongana uso kwa uso na roli aina ya fuso Desemba 24, saa 9 mchana  na marehemu walizikwa jana katika eneo la Kiwanja cha  Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga, Parokia ya Kahama Mjini mkoani Shinyanga.

Misa ya mazishi  imefanyika katika Kanisa Kuu la Jimbo na  imeongozwa na Askofu Fravian Kasala wa jimbo Katoliki Geita, pamoja  na Maaskofu  Liberatus  Sangu wa Shinyanga, Joseph Mlola wa Kigoma  na mwenyeji Askofu Ludovick Minde wa jimbo Katoliki la Kahama.