
Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ni Denis Onyango kutoka Uganda na klabu ya Mamelodi Sundowns.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa kuamkia leo limetoa tuzo kwa wachezaji, timu na waamuzi waliofanya vizuri katika sekta hiyo kwa mwaka 2016.

Hafla hiyo iliyofanyikia nchini Nigeria ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka lakini pia ikiwa imepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwe Diamond Platnumz na Rayvanny kutoka nchini Tanzania.

Mchezaji Bora wa Kike ni Asisat Oshoala kutoka Nigeria anayekipiga katika klabu ya wanawake ya Arsenal.
Wachezaji na timu mbalimbali zilitajwa kuwania tuzo katika vipengle mbalimbali, lakini hapa chini ni orodha ya washindi kutoka katika vipendele hivyo.

Tuzo ya Klabu Bora ilinyakuliwa na Mamelodi Sundowns F.C kutoka Afrika Kusini baada ya kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika wakati Timu Bora ya Taifa ya Wanaume ikitajwa kuwa ni timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Tuzo ya Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ilikwenda kwa timu ya Nigeria, Super Falcons baada ya kutwaa kombe la AFCON kwa mara ya 8.

Mwamuzi Bora ni Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia

Kikosi Bora cha Mwaka 2016

Kocha Bora wa Mwaka 2016 ni Pitso Mosimane kutoka Afrika Kusini.

Tuzo ya ‘Most Promising Talent’ ilikwenda kwa Kelechi Iheanacho kutoka Nigeria anayeichezea Man City.
#GloCAFAwards2016 Winga wa #LeicesterCity na timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez ametajwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa mwaka 2016. pic.twitter.com/myh04iMBnS
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017
#GloCAFAwards2016 Denis Onyango kutoka Uganda ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani. pic.twitter.com/8C7Dl4tAoy
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017
#GloCAFAwards2016 Asisat Oshoala kutoka Nigeria anayechezea timu ya wanawake ya #Arsenal atajwa kuwa Mchezaji Bora Afrika kwa Wanawake. pic.twitter.com/bzSn2tXSHL
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017
#GloCAFAwards2016 Klabu Bingwa Afrika, Mamelodi Sundowns F.C. kutoka Afrika Kusini imetajwa kuwa Klabu Bora Afrika mwaka 2016. pic.twitter.com/D5bU103TYh
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017
#GloCAFAwards2016 Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria imetwaa tuzo Timu Bora ya Taifa ya Wanawake baada ya kushinda kombe la AFCON mara 8 pic.twitter.com/DvkQBdSYmp
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017
#GloCAFAwards2016 Timu ya taifa ya Uganda, The Cranes wameshinda tuzo ya Timu Bora ya Taifa ya Wanaume mwaka 2016. pic.twitter.com/k9wjw6oHsk
— Global Publishers (@GlobalHabari) January 6, 2017