×

Kutokwa na vinyama sehemu za siri (genital warts) kwa wanawake

genital-warts-pictures-500x332 KUTOKWA na vin­yama, mafindofindo yanayoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri (genital warts) ni ugonjwa unaoenezwa kwa kujamiiana na kitaalam hu­itwa Sexually Transmitted Infection kifupi STI.

Ugonjwa huu unaweza kuto­kea kwenye uke, mrija wa mkojo (urethra), shingo ya kizazi (cervix) au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.

Ugonjwa huu husababishwa na jamii ya virusi viitwavyo kitaalam Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo vipo zaidi ya aina 70 tofauti ingawa si wote wanaosababisha ma­radhi haya ya maeneo ya siri.

Aina nyingine za HPV hu­sababisha kutokwa na vin­yama kwenye ngozi inayo­zunguka sehemu nyingine za mwili kama kwenye mikono au miguu.

Baadhi ya aina za virusi vya HPV, pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi ambayo kitaalam huitwa Carcinoma of the Cervix kwa wanawake au saratani ya haja kubwa, kwa jinsia zote.

Ugonjwa huu wa kuota vin­yama sehemu nyeti umejitoke­za kwa kasi kubwa na watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile.

Kwa upande wa wanawake, virusi wa HPV vina uwezo wa

kusambaa hadi maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi (cervics) bila dalili kujitokeza.

Kama tulivyoeleza, maam­bukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni.

Mara baada ya kuam­bukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa ugonjwa wa kuo­ta vinyama kuji­tokeza wazi, i n g a w a b a a d h i ya wag­o n j w a w a ­naweza k u k a a h a t a m i a k a k a d h a a bila kuwa n a d a l i l i yoyote.

Watu ambao wa­naweza kukumbwa na maam­bukizi ya ugonjwa huu ni wale wenye wapenzi wengi wa­naofanya ngono isiyo salama, kufanya ngono katika umri mdogo na walio na maam­bukizi ya Virusi vya Herpes na wakati huohuo kuwa na msongo mkali.

Walio na upungufu kati­ka mfumo wa kinga mwilini

 kwa sababu ya magonjwa mbalimbali au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani wanaweza kupata maradhi haya.

DALILI

Kuota vinyama vidogo au genital warts huonekana kama vioteo laini vinavyoji­tokeza juu ya ngozi ingawa wakati mwingine vinaweza kuwa vidogo mno kiasi cha kutoonekana vizuri kwa ma­cho ya kawaida.

Dalili nyingine ni mgonjwa kuwa na ganzi maeneo yaliy­ozungukwa ugonjwa na kwa wanawake, uchafu unaotoka sehemu za siri huongezeka na atakuwa anawashwa sana maeneo ya siri na wakati mwingine kutokwa na damu ukeni mara baada ya tendo la ngono. Hata hivyo, ni kwa baadhi tu ya wanawake.

Kwa upande wa wanawake pia ugonjwa huu hujitokeza ndani ya uke au njia ya haja kubwa, nje ya uke au ngozi ya nje kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani ya uke kuzunguka eneo la shingo ya kizazi.

ITAENDELEA