The House of Favourite Newspapers

Madee Kupora Simu ni Kiki?

madeee2

Madee.

DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita siku chache tangu msanii wa bongo Fleva na staa wa wimbo ya Pombe, Hamad Ally ‘Madee’ kudaiwa kumpora simu mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Makavaka maeneo ya uwanja wa ndege Julius Nyerere Dar es Salaam.

madee1

  Katika mitandao ya kijamii mapema leo zimesambaa picha zikionesha wimbo mpya wa Madee uitwao ‘Hela’. Wadau na mashabiki wa Bongo Fleva wamehusisha ‘skendo’ ya Madee kupora simu na ujio wa wimbo wake mpya ambao utasikika leo katika vituo mbalimbali vya redio. Skendo hiyo imeonekana kama ni kutafuta ‘Tention’ ili aweze kutoa kibao chake kipya.

madee4

Wimbo huo umeandaliwa katika studio za ‘Mj Record’  kwa ushirikiano wa waandaaji wawili ambao ni Marco Chali na Daxo Chali.

Salum milongo/GPL

 

Comments are closed.