×

Tanzania na Uturuki Zatiliana Saini Mikataba 9 ya Makubaliano ya Kiuchumi

magufuli-na-erdogan-1

 Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wao Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo. Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.

magufuli-na-erdogan-2

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwalaki Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mazungumzo.

magufuli-na-erdogan-3 magufuli-na-erdogan-4

 RaisPombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan wakipiga ngoma Ikulu jijini Dar, leo.

Akizungumza mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na kimaendeleo baina nchini hizo.

magufuli-na-erdogan-5

 Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwazawadia Kinyago cha Umoja na Mchoro wa Mlima Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar, leo.

Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.

magufuli-na-erdogan-6

 Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli na mke Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mama  Emine Erdogan wakipeana mikono baada ya maongezi  Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.

magufuli-na-erdogan-7

 Rais Erdogan akiongea baada ya yeye na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli kushuhudia uwekaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Uturuki Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari  23, 2017.

Rais magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

magufuli-na-erdogan-8

 Rais Magufuli na akihutubia wakati wa kongamano hilo.

Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.

magufuli-na-erdogan-9

 RaisErdogan  (kulia) akishikana mkono na mwenyeji wake, Rais Magufuli.

Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.

magufuli-na-erdogan-10

 Rais Erdogan  akihutubia wakati wa kongamano hilo.

“Kiwango cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais huyo.Aidha Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.

magufuli-na-erdogan-11

 Rais Erdogan  akiongea na mwenyeji wake Rais Magufuli.

Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.

magufuli-na-erdogan-12

 Rais Erdogan  na mwenyeji wake Rais Magufuli wakishuhudia ubadilishanaji hati baada ya kusaini baina ya mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa sekta binafsi Dkt Reginald Mengi na kiongozi wa msafara wa wafanyabiashara wa Uturuki katika kongamano hilo.

PICHA NA IKULU

Prof. Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini.