WIZARA ya Afya imesema wagonjwa wapya wawili Watanzania wamethibitika kuwa na virusi vya Corona (COVID-19) jijini Dar es Salaam, na mmoja aliyeripotiwa jana kutokea Zanzibar, hivyo jumla ya wagonjwa wa #CoronaVirus waliothibitika nchini mpaka sasa wamefikia sita.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na wizara hiyo leo Machi 19, 2020.

