
UFILIPINO: LILE Shindano la 65 la kumsaka mrembo wa dunia, Miss Universe limemalizika nchini Ufilipino ambapo mrembo Iris Mittenaere raia wa Ufaransa ameibuka mshindi namba moja wa taji hilo huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Raquel Pelissier raia wa Haiti kupitia kwa na namba 3 akiwa ni Andrea Tovar raia wa Colombia.
Licha ya washindi kupatikana, shindano hilo lilikuwa lenye mvuto na msisimko hasa ukizingatia Afrika ikiwemo Tanzania ziliwakilishwa na warembo wake Jihan Damack.
Kwa upande wa Afrika Mashariki na Afrika nzima, Kenya ilifunika wakati wa mchujo baada ya mrembo wake, Mary Esther Were kutangazwa kuingia kwenye 9 bora ya dunia akiwa ni Mrembo pekee wa Afrika kuingia Top 9.

Miss Universe Tanzania 2016, Jihan Dimachk
Wakati mchujo huo ukiendelea, Waafrika waliongeza hamasa zaidi baada ya Mrembo huyo wa Kenya kutangazwa tena kuingia kwenye 6 bora ambapo licha ya kuondolewa kwenye 3 bora.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ
Endelea kutembelea website ya Global Publishers kila siku, tutaendelea kukusogezea kila news inayotokea mahali popote duniani.