
Belle 9
MWANAMUZIKI anayetamba kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’, amefunguka kuwa amebakiza mambo mawili tu kwenye muziki ambayo akiyakamilisha, atamshukuru Mungu na atanyoosha miguu kufurahia maisha yake ya muziki kwa muda wote aliokomaa kwenye gemu.
Akichonga na Global Publishers, Belle 9 ambaye wimbo wake waI unafanya vizuri kwenye gemu, amesema mambo hayo ni pamoja na kumiliki bendi na studio ya ndani ya nyumbani kwake.
“Nimefanya mambo mengi sana kwenye gemu, nikifanikiwa kukamilisha hayo tu, basi nimemaliza, yatakuwa ni matunda makubwa ambayo nitakuwa nimepata kupitia muziki,” alisema Belle 9.
Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, January 31, 2016. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.
Kwa stori zote kali, Tu-follow
Facebook @Globalpublishers
Twitter @GlobalHabari
Instagram @GlobalPublishers
YouTube @GlobalTVTZ