



KUFUATIA kuanza kwa mchakato wa Bahati Nasibu ya awamu ya pili ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers & General Interprises, kupitia magazeti yake ya Championi,Risasi,Amani, Uwazi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, mapema leo wakazi wa Chaninika wameonyesha hali ya kupagawa baada ya timu nzima ya promosheni hiyo kutua mtaani kwao.
Timu hiyo iliwasili mapema leo Chanika, na kuanza kuanza kufanya mauzo ya magazeti yake kwa lengo la kuwawezesha wakazi wa eneo hilo kununu gazeti kisha kujipatia kuponi inayoweza kuwawezesha kuibuka na nyumba hiyo ya kisasa kabisa.
Chanika ni eneo ambalo limeendelea kuonyesha kiu ya wasomaji wengi wa jiji la Dar es Salaam, kuwa na shauku ya kujishindia mjengo huo wa kisasa ambao utatolewa ndani ya mwaka huu, huku droo ya kwanza ya bahati nasibu hiyo ikitarajiwa kufanyika jumatano ya wiki ijayo 8/2/2017.
Na Musa Mateja