×

Jack Chuzi Apigwa Talaka Tatu

Stori: MAYASA MARIWATA| AMANI

 ALIYEKUWA mume wa staa wa filamu Bongo Jack Pentezel ‘Jack Chuz’ ambaye ni mfanyabiashara Gadner Dibibi amesema kuwa, aliamua kumpa mkewe talaka tatu baada ya kuona amemdhalilisha mitandaoni kwa matusi ya nguoni pamoja na kumuanika mwanaume mwingine aitwaye Chris.

Akibonga na paparazi wetu Dibibi alisema, awali walivyotibuana hakuwa amempa talaka zote na wala alikuwa hajafikiria hicho kitu sababu kinahitaji kujitafakari kwa muda mrefu na kufanya uamuzi sahihi usio na majuto, lakini kwa kilichotokea akaona wakati muafaka umefika.

“Nimeshampa Jack talaka zote tatu hivyo yupo huru kuolewa kama na huyo Chris au mwanaume yeyote yule uamuzi ni wake, sifikirii kuoa kwa sasa nahitaji kujipanga zaidi ili kupata chaguo sahihi na wala sitakuja kuoa msanii tena nahitaji mtu wa kawaida tu,”alisema.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save