

MAMA mzazi wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu amezidiwa baada ya kupandwa na presha wakati alipokwenda katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar (Sentro) kwa ajili ya kumuona mwanaye ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi pamoja na wasanii wenzake kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Katika hali hiyo, mama Wema aliishiwa nguvu na kusaidiwa na ndugu wawili waliokuwa wameambatana naye kituoni hapo na kutolewa nje ya lango kuu la kituo hicho kisha muda mfupi baadaye akaonekana akiondoka eneo hilo.
PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS