×

Shoga; Kumbuka Huu ni Mwezi Mubashara!

HAYA sasa shoga yangu sema wewe maana nikisema mimi utasema nasingizia, nasengenya, naona wivu, upo? Ni Jumanne tena nyingine tulivu kama tulivyoachana mwezi jana tumekutana tena mwezi huu, mwezi wa mashamsham, mwezi wa mubashara na mpenzi wako, mwezi wa yale mambo yetu ya maua, manukato, saresare, ehee hee hee heiyaa!

Nicheke miye, nikinuna unadhani utanisoma, utanielewa? Shoga mwenzako kiafya nipo fiti nimejaa tele kama jumba la sinema, hofu kwako unayenisoma ila kama ni mzima jambo la kumshukuru Muumba lakini kama unaumwa pia kuombeana ni kitu muhimu kwani leo wewe kesho mwenzako!

Shoga yangu baada ya hayo nigeukie kwenye kileee kilichonifanya nikuandikie yote haya, kilichonifanya kutoka povu la bia na siyo la sabuni, upo? Kama utakumbuka shoga yangu wiki iliyopita nilizungumza na wale wenzangu na mimi ambao ukifika muda wa chakula cha usiku wao ni kukimbilia kula gizani, loo!

Hata tone la aibu huna shosti sijui braza wewe! Sijui wa wapi wewe au ndo tuseme umekula maharage ya wapi? Unapenda vya gizaaani mbona ukisema upewe hela gizani hutaki, Shuuu! Shoga siku hizi mapenzi ni kidijitali, mnakula chakula chenu vijiko vinagongana mnaviona kabisa, umenipata?

Basi shoga yangu acha nipate mimeseji hiyo! Wapo walionijia juu eti nawaumbua sana. Hebu ngoja niongeee na mwana wewee ambaye unaendekeza zama za kizamani, yaani mimi nikuumbue kwa kusema ukweli? Kwa mchepuko unataka kula chakula kwenye mwanga lakini kwa mkeo/ mumeo unataka kula kwenye giza, inahu! Wenzako kila siku wanagombana kwenye ndoa zao na wengine wanasema hawasikii ladha ya chakula kisa kila ukifika muda wa kukila wanataka taa izimwe, looo!

Pole yako!

Basi shoga yangu acha nielekee kwenye mada yetu ya leo, mwenzako mie, msamaria mie, mwana kila kitu mie, wakusuluhisha kama siyo kufundisha si nimepokea tena meseji ya malalamiko eti tangu mwaka umeanza mtu amenuniwa, heee! Nachoka mie!

“Habari yako dada Sophy! Dada mwenzako nimeumaliza na kuuanza mwaka vibaya. Mimi ni mama wa watoto wawili mmoja nje ya ndoa. Dada katika uhusiano wetu tuna zaidi ya miaka mitatu lakini kilichonifanya niyaongee haya hapa, tangu tumemaliza na kuanza mwaka mwenzangu simuelewi. Ilikuwa kawaida yetu kula chakula kila baada ya siku tatu hadi nne kutokana na majukumu yetu kwani kazi tunazofanya ni ngumu ati.

“Sasa tangu tumemaliza mwaka na kuingia mwingine mume wangu amenibadilikia, hataki kabisa kusikia kitu kinaitwa chakula cha usiku. Yupo tayari alale na njaa ifikapo usiku na hapa ninapokwambia huu unaenda mwezi wa pili hajui vijiko wala vikombe vyangu vipoje, shoga nahitaji ushauri nahisi labda kapata sehemu nyingine ya kula chakula hicho usiku akirudi analala amechokaaa, nikiongea naye anakuwa mkali kweli!” meseji hiyo amenitumia msomaji wangu.

Shoga yangu kwanza nikupe pole yako na umwambie huyo mwanaume ndoa hazipo hivyo. Na wewe usije kujaribu kuhamisha majeshi kwa mwingine, kaa naye chini mjadiliane, ikitokea kila mkikaa naye chini hataki kusikia basi taratibu unaanza kushirikisha ndugu.

Mwezi mubashara huu

Shosti kingine anatakiwa kuangalia huu ni mwaka mwingine tena na mwezi mwingine na kama unavyosikia mwezi huu ni wa mubashara kwa wale wapendanao! Mwezi huu ni wa kuonesha kumpenda na kumuonesha kujali kweli. Ukiachana na zawadi, mwezi huu ndiyo wa kupanga mambo yenu kimahusiano, upo? Ongea naye najua mtafikia pazuri.

Nguo ya jirani

Niwageukie nyie wengine ambao mwezi huu mnautumia vibaya. Shoga kwanza unatakiwa utambue nguo ya jirani haivuliwi. Najua umetoa macho kodo hujui hiyo nguo ya jirani ni ipi? Shoga usitake tumwage mchele kwenye kuku wengi, nguo ya jirani ni mchepuko.

Ngoja nikung’ate tu sikio wangu, mwezi kama huu siyo wa kumuacha mwenzi wako aende kwa mchepuko, upo? Tulia na mwezio, hizi tamaa sijui ameumbwa tofauti na wako, achana nazo!

Mwezi wa usafi

Kama ulikuwa hujui nakupasha sasa! Shoga mwezi huu ndiyo wa kumfanya umpendaye asijute umenipata! Kama ulikuwa umejisahau sehemu f’lani katika mwili wako basi jirekebishe, fua, safisha!

Kwa leo niishie hapa shoga yangu, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Save