STORI: Na IMELDA MTEMA| RISASI JUMAMOSI|DAR ES SALAAM
KUFUATIA kuwepo kwa hofu ya mastaa zaidi kutajwa kwenye listi ya watu wanaojihusiha na madawa ya kulevya, Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ alijikuta akitoka povu la aina yake kumjibu shabiki aliyemtania kuwa msanii huyo naye yupo kwenye listi.
Lulu alimwaga povu hilo katikati ya wiki hii wakati ‘homa’ ya madawa ya kulevya ilivyokuwa juu jijini Dar baada ya mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda kulivalia njuga suala la madawa ndipo shabiki mmoja wa msanii huyo kupitia Mtandao wa Twitter alipomtibua Lulu.
Shabiki huyo anayetumia jina la MwanaMonduli aliandika; “Dada tulia maana na wewe upo kwenye listi.”
Baada ya kuandika hivyo, Lulu alifyatuka maneno makali ambayo hayaandikiki gazetini. Risasi Jumamosi lilimcheki kupitia simu yake ya mkononi, akasema amemchana shabiki huyo kwani watu wa aina hiyo wamekuwa wakimkwaza hivyo amempa dawa.