×

Watakaokunywa Pombe Simba, Yanga Kukiona!

Kamanda Sirro

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, limesema kuwa, limejipanga vilivyo kuhakikisha usalama wa raia  unakuwa salama kwa kupambana na watakaoingia kwenye mechi ya Simba na Yanga kesho wakiwa wamelewa pombe.

Hayo ameyasema leo Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro ambapo mchezo huo wenye mvuto unaosubiriwa kwa shauku kubwa nchinib Tanzania na Afrika Mashariki utachezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho siku ya Jumamosi.

“Wananchi wasiwe na wasiwasi wowote  wa kiusalama  na pia watoe ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa ya jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa ndani ya uwanja au nje.

“Ole wao wale waliozoea kuvunja viti vilivyomo ndani ya uwanja huo wajitokeze, watakiona na tutawashughulikia kwelikweli,” alisema Sirro.

Aliongeza kuwa, katika mageti yote ya kuingilia mashabiki kutakuwa na vifaa maalum vya kupima vileo (pombe) kwa yeyote na atakayebainika hataweza kuruhusiwa kuingia uwanjani.

Na Denis Mtima/GPL