The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Dogo Janja Alizwa, Ni Baada Ya Kutoka Moshi Kwenye Killimanjaro Marathon – (Video)

Camera za Global TV Online zimekutana na msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja na kupiga nae stori mbili tatu, lakini katika maongezi yetu msanii huyo wa HipHop alionekana kukosa raha na baada ya kumdadisi tukagundua kuwa gari yake ilipata msala weekend hii iliyopita.

Dogo Janja ameifungukia Global TV Online na kutuambia jinsi ilivyokuwa mpaka taa za mbele na nyuma na baadhi ya vifaa vya ndani ya gari yake kama radio kuibiwa… akizungumza na camera zetu msanii huyo alifunguka na kusema:

>> “Jana nilienda Moshi, nilikuwa na show ya Kili Marathon na baada ya kufanya show mchana usiku niligeuza kuja Dar es salaam, lakini inaonekana kuna watu walikuwa kwenye rader yangu wananifuatilia….“<<- Dogo Janja.

>> “… wamepiga power window, taa za mbele na za nyuma, na radio yaani wamepiga nyang’anyang’a. Asubuhi  naamka nimekuta gari inanizomea nilikuwa nahisi kama naota, nikawa nafikicha macho kuhakikisha…“<< – aliendelea kuelezea Dogo Janja.

Hizi ni baadhi ya picha za gari la Dogo Janja sasa.

Isitazame interview yake nzima hapa chini akielezea kwa masikitiko jinsi ilivyokuwa…

 

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasia, michezo, comedy, burudani, muziki na mengineyo yakufikie  kwa wakati.

Comments are closed.