
MABINGWA watetezi wa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara, Young African Sc (Yanga) wameendeleza hasira zao kwa kuitwanga klabu ya Kiluvya United kwa mabao 6-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ulioigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kusisimua, Kiluvya walianza kwa kasi huku wakigongeana pasi zakaribu karibu kumbe Yanga walikuwa wakiwasikilizia tu.

Hali ilibadilika kunako dakika ya 10 baada ya Yanga kujipatia bao la kwanza kupitia kwa Geofrey Mwashiuya.

Dakika 12 baadaye mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akafumania nyavu za Kiluvya United kunako dakika ya 22 na kuiandikia Yanga bao la 2 huku.
Dakika ya 40, Edgar Charles akaiandikia Kiluvya bao la kufutia machozi.

Chirwa akiwa na uchu wa mabao akafumania tena nyavu za Kiluvya United kunako dakika ya 45 na kwenda mapumziko Yanga wakiongoza kwa bao 3-1.

Kipindi cha pili Yanga hawakuridhika na bao hizo 3, wakakaza tena.
Yanga hawajatosheka, Chirwa akarudi tena dakika ya 71 na kuandika bao la 4.

Dakika ya 76, Juma Mahadhi anaiandikia Yanga bao la 5.

Chirwa huyo huyo akamaliza mchezo kwa kuandika bao la 6 kunako dakika ya 87.


Hadi mchezo unamalizika, Yanga 6-1 Kiluvya United.

Chirwa ameonekana staa kwa mchezo wa leo huku peke yake akifunga bao 5 na kuondoka na mpira wa zawadi.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS