
BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa tathmini yake katika kusimamia shughuli za utunzaji wa mazingira nchini chini ya sheria ya Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.


Hayo yameelezwa leo na Ofisa Mkuu wa Mazingira (NEMC), Arnold Kisiraga alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo pia alisema kuwa NEMC inayo mamlaka ya kukuza, kuchochea, kusimamia na kuunganisha masuala yote yanayohusiana na mazingira.

Alifafanua kuwa baraza linawajibika kuhakikisha kuwa mazingira yanatunzwa ili kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali, ustawi na maisha bora ya wananchi na ukaguzi wa mazingira na kutoa maelekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha hali ya mazingira au kutoa makatazo mbalimbali ya kisheria yenye kudhibiti uchafuzi na uharibifu wa mazingira kutoka katika baadhi ya viwanda visivyozingatia sheria ya mazingira.