Waziri Mkuu Mstaafu. Jaji Joseph Warioba akizindua kitabu.




Waandaji wa kongamano hilo ni mtandao wa wanawake na katiba, uchaguzi na uongozi.

Mwakilishi kutoka Mtandao wa WFT Prof. Ruth Meena


WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa Watanzania wanapaswa kupiga vita madawa ya kulevya ili kuwa na kizazi bora ambacho ni nguvu kazi ya Taifa.
Hayo ameyasema leo wakati alipokuwa katika Kongamamano la Wanawake na Wasichana Katika Uongozi Tanzania na Uzinduzi wa kitabu cha historia ya Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Warioba ameongeza kuwa, Wanacnhi wanapaswa kuiunga mkono serikali katika kupambana na wanaohusika kulima vilimo vya bangi sambamba na matumizi ya dawa za kulevya.
“Ipo haja kwa watanzania kuyajengea nguvu ya pamoja mambo muhimu ya kitaifa ili kuyafanikisha, huku akigusia suala la uwepo wa dalili ya uhaba wa chakula na vita dhidi ya dawa za kulevya,”
“Tatizo la dawa za kulevya linazungumzwa kama jambo la kawaida, badala yake tumetafuta mchepuo wa kisiasa, ambao ndio unazungumzwa” alisema Warioba.
PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS