×

Genevieve Aolewa, Atundikwa Mimba

Genevieve Nnaji

Na ANDREW CARLOS| GAZETI LA IJUMAA| KUTOKA NAIJA

KONGWE wa filamu kutoka Nollywood, Genevieve Nnaji anadaiwa kuolewa kisirisiri akiwa ametundikwa mimba. Kwa mujibu wa chanzo, Genevieve aliyewahi kutikisa na filamu ya Most Wanted, amefunga ndoa hivi karibuni katika kisiwa kimoja nchini Nigeria huku jina la mumewe bado likiwa siri.

Genevieve Nnaji

Kuonesha kuwa hataki kujitokeza hadharani kutokana na tumbo lake kuanza kuwa kubwa, juzikati aligomea kuhudhuria sherehe za utoaji tuzo za filamu za Africa Magic Viewers’ Choice (AMVCA) ambazo hajawahi kutoshiriki kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo tangu zianze kutolewa.

Kwa sasa staa huyo aliyeanza kuigiza akiwa na miaka nane, ana  mtoto mmoja, Chimebuka aliyemzaa na mwanaume mmoja ambaye ni raia wa Marekani akiwa na miaka 18 tu.