×

VIDEO: Umeipata Hii Exclusive ya Diamond Kuuza Nyimbo za Wasanii Wote wa Africa?

LEBO ya Muziki hapa Bongo inayomilikiwa na Diamond Platinumz, Wasafi Classic Baby (WCB) imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa kwenye tasnia hiyo ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo ya kiteknolojia kwa ajili ya kuuza nyimbo mbalimbali za wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

WCB wamebuni website mpya ya wasafi.com ambayo ndani yake msanii ataweza kuweka wimbo wake na kuuza kwa njia za kiteknolojia kupitia njia mbalimbali za malipo ikiwemo mifumo ya mitandao ya simu pampja na mifumo ya kibenki.

Taarifa hiyo njema ameizungumza Diamond mwenyewe wakati akipiga stori na familia ya Global TV Online juzi, Jumamosi, Machi 11, 2017.

Diamond amesema kupitia website hiyo pamoja na App itakayozinduliwa hivi karibuni, wasanii wote wa Tanzania, Afrika na Dunia, kwa anayependa atakuwa na uwezo wa kutupia ngoma yake pale, akauza online na kujipatia mtonyo pamoja na kuonza mauzo yake na kazi za wasanii wengie.

Msikie Diamond akifunguka.