
Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati nchini. Dkt. Said Sima (kulia) akisoma hotuba yake mbele ya mgeni rasmi.

Mmoja wa wadau wa somo la hisabati kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma, Andrew Binde, akizungumza.

Meza kuu ilivyoonekana.

Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.

Hassan Lissu, ambaye alikuwa mgeni rasmi akikabidhi vyeti na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika somo la hisabati kwa shindano lililofanyika mwaka jana.



WANAFUNZI nchini wametakiwa kulipa kipaumbele somo la hisabati kutokana na umuhimu wake katika jamii. Wito huo ulitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati nchini. Dkt. Said Sima, aliyesema wanafunzi wengi bado wanafeli somo la hisabati, kwa hiyo kuna haja ya wadau mbalimbali kuwahamasisha wanafunzi na watu wengine kulipenda somo hilo.
“Serikali iweke kipaumbele katika kuwapatia walimu wa somo la hisabati posho na kuwaongezea mishahara, pia iweke msisitizo wa wanafunzi kujijengea klabu za wanafunzi pamoja na sera imara katika kushughulikia masomo ya hesabu,” alisema.
Maadhimisho ya Pai Tanzania yamefanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUSE) jijini Dar es Salaam, lengo lake likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kulipenda somo la hisabati ambapo kauli-mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni “Hisabati ni Msingi wa Sayansi na Teknolojia”.
Mgeni rasmi wa maadhimsho hayo alikuwa Hassan Lissu ambaye ni Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
NA DENIS MTIMA/GPL