
ILE Droo ya Pili ya Shindano kabambe la Shinda Nyumba Msimu wa Pili iliyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, imefanyika leo katika Viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo washindi wanne wamepatikana baada ya droo hiyo kuchezeshwa sehemu ya wazi kama ilivyo kawaida ya mashindano ambayo huandaliwa na Global Publishers.

Washindi hao ni kama ifuatavyo;
Mshindi namba 1 ni; Victor Mubi, Mkazi wa Mwenge Dar es Salaam ambaye amejishindia Pikipiki mpya.
Mshindi namba 2 ni; Josephine Boniface mkazi wa Songea, ambaye amejishindia TV Flat Screen mpya.
Mshindi namba 3 ni; Ramadhani Zuher Naguli, Mkazi wa Morogoro ambaye amejishindia simu, SmartPhone.
Mshindi namba 4 ni; Rose Wilbert Mlay Mkazi wa Kunduchi, Dar es Salaam ambaye amejishindia Dinner Set.

Mnenguaji akifanya yake jukwaani.
Wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers, wakichangamkia Gazeti la Ijumaa na Championi kabla ya Droo ya Pili ya Shinda Nyumba kuanza mapema leo.
Mr. Shinda Nyumba katika pozi na wasomaji wa magazeti ya Global Publishers.
Kuponi zikichanganywa ili kutafuta washindi wa Droo ya Pili ya Shinda Nyumba.
Msomaji akizibwa uso ili asionse kuponi atakayoichagua kati ya rundo la kuponi. 
… Akisoma jina la mshindi.
Kuponi zikichanganywa.
MC. Chaku akimpigia simu hadharani mshindi wa pikipiki kwenye droo ya pili ya shinda nyumba.


Kutoka kulia ni wawakilishi kutoka Kampuni ya Global Publishers ambao pia ni wahariri, Sifael Paul na Elvan Stambuli, Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein (katikati), Afisa Uhusiano wa Global Publishers, Soud Kivea pamoja na Ofisa Masoko, Yohana Mkanda wakifuatilia tukio hilo.

Mr. Shinda Nyumba akitoa zawadi ya flana kwa mshindi.



Burudani zilivyonoga.