×

VIDEO: Rais Magufuli Azindua Rasmi Ujenzi wa Flyover ya Ubungo Dar

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezindua rasmi Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Juu kwenye Makutano ya Ubungo (FlyOver ya Ubungo) itakayoanza kujengwa hivi karibuni.

Akiuelezea mradi huo Rais Magufuli amesema Ujenzi wa barabara juu ya Ubungo utatumia miezi 30 kukamilika na utagharimu jumla ya TZS bilioni 188 ambapo bilioni 186 zinazotolewa na Benki ya Dunia (WB) na zingine zitatolewa na serikali ya Tanzania.

Aidha Fly-Over ya Ubungo itakuwa na (ghorofa) njia tatu, njia ya chini, ya kati na juu. Ambapo njia ya chini itakuwa ni ya Morogoro – Mjini Kati, Barabara ya juu itakuwa ni kwa ajili ya gari za Mwenge – Tabata huku njia ya kati itakuwa makutano kwa wanaohitaji kubadili njia.

Kwa upande wake, Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dkt. Jim Kim ambao ni wafadhili wakuu wa mradi huo, wamejidhatiti kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.

TAZAMA VIDEO HAPA JPM AKIFUNGUKA