×

Watanzania na Wachina washerehekea wiki ya Filamu za China

Nape akizungumza kwenye hafla hiyo.

KAMPUNI ya StarTimes Tanzania, jana Jumatano iliwakutanisha Watanzania na Wachina katika kusherehekea Wiki ya Filamu za China kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar.

Nape akizungumza kwenye hafla hiyo.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wasanii kutoka Tanzania na China, mgeni rasmi alikuwa Nape Nnauye ambaye awali alikuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, kabla ya kutenguliwa uteuzi wake.

Baadhi ya wahudhuriaji wakiwa katika hafla hiyo.

“Wachina ni ndugu zetu na hatuna budi kujumuika nao katika kusherehekea Wiki ya Filamu za China ambapo ni furaha kwetu kuona baadhi yao wakijua kuzungumza Kiswahili.

Nape akiwa na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang.

“Tunachotaka kufanya sasa ni kuzitafsiri filamu za Kitanzania kwa Lugha ya Kichina ili ndugu zetu hawa waweze kuziangalia kule kwao kama ilivyo kwa filamu zao zilizotafsiriwa kwa Kiswahili,” alisema Nape.

Nape akizungumza na wanahabari.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Tong Gang, alisema: “Ni faraja kwetu kuona tunadumisha undugu ambao ulianzishwa na babu zetu huko nyuma, sisi kama warithi tunapaswa kuuendeleza na kwa kupitia filamu naamini tutafanikisha hilo.”

Mwigizaji maarufu wa China, Feng Wen Juan ‘Maudodo’ akiwa na Tong Gang.

 

Tong Gang akikata utepe katika hafla hiyo.
Tong Gang akizungumza katika hafla hiyo.

PICHA: DENIS MTIMA